Wakati huo huo Umoja wa Mataifa unasema kuwa wastani wa watoto wanaozaliwa na mwamamke mmoja dunia utapungua hadi watoto wawili kufikia mwaka 2100. Wastani wa watoto wanaozaliwa na mwanamke mmoja wa Kiafrika kwa sasa ni 4.7 ikilinganishwa na Ulaya ambapo kiwango hicho ni 1.6. Makadirio ya Umoja wa Mataifa yanasema hadi kufikia mwaka 2100 watu wa bara Afrika watakuwa zaidi ya mara tatu ya wakazi wa sasa wa bara hilo na kufikia bilioni 3.6. Hali hii inasababishwa na ongezeko la watoto wanaozaliwa kila siku barani Afrika ikilinganishwa na Ulaya ambako idadi inapungua siku baada ya siku.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 274735
Abna inatuarifu kuwa:Leo Umoja wa Mataifa unajitayarisha kutangaza takwimu ya idadi ya watu duniani ambayo inasadikiwa imefika bilioni saba baada ya kuongezeka mara sita katika kipindi cha miaka mia mbili iliyopita. Makadirio ya kimataifa yanasema kuwa idadi ya watu duniani itakuwa zaidi ya watu bilioni saba kufikia mwaka 2050 na kupita bilioni 10 kufikia mwishoni mwa karne ya sasa.